FAIDA 7 ZA KUOGEA SABUNI YA MCHELE KWA WANAWAKE

 

        "Urembo wa Asili ndio Urembo wa Bora Zaidi"

 Je! unafahamu kuwa asili (nature) imekupatia njia bora na  salama ya kukufanya uonekane mrembo bila kulazimika kutumia kemikali ambazo zinaweza kukuletea madhara  kiafya? 

     👉 Kama hufahamu hilo, usiwe na wasiwasi kwa kuwa katika makala hii nitakuonesha jinsi ambavyo utumiaji wa sabuni ya mchele wakati unaoga itakufanya uonekane mrembo bila kujichubua na vipodozi ambavyo vimewekewa kemikali zenye sumu.  

     👉 Inawezekana ukawa miongoni mwa watu ambao wanashagaa kuwa inawezekanaje mchele ukawa na uwezo wa kukufanya uonekane mrembo? Au inawezekana ukawa ni miongoni mwa wale ambao wanakadhani labda nimekosea na hivyo unatamani kusikia nikifuta kauli yangu. 

      👉  Nakuhakikishia kuwa sijakosea na kauli hiyo siiifuti ng'ooo kwa kuwa nina uhakika na ninachokiandika. 

     👉   Kinachonifanya niwe na uhakika na hiki ninachokisema ni  kutokana na historia kutudhibitishia hilo. 

👂👂 Tega sikio lako vizuri ili nikupe hiyo historia kama hautajali. Toka enzi za mababu mchele umekuwa ukitumika kama kitu maalumu cha kuwafanya wanawake waonekane warembo na kwa kipindi hicho neno lililokuwa linatumiwa sana "vigori"

  👉 Kipindi hicho makabila mengi walikuwa na kawaida ya kuwaweka unyagoni mabinti pale tu wanapopevuka. Wakati ambao mabinti hao wakiwa ujagoni, moja ya kitu kilichokuwa kinafanyika ni kuwasafisha miili yao  kwa maji ya mchele.

" Najua kwa wale wahenga watakuwa wanakumbuka jinsi ambavyo walikuwa wanatumia maji ya mchele kusafisha nyuso zao kwa kutumia maji ya mchele ili kuzuia chunusi zilizokuwa zinatokea usoni kwao kipindi walipokuwa wanapevuka "

     👉 Lengo kubwa la kufanya hivyo lilikuwa ni kuifanya miili yao iwe na muonekano  mzuri (warembo) ili siku wakitolewa kila mmoja hasa wanaume apagawe kutokana na urembo walio nao. 

     👉Hata leo hii kuna bidhaa nyingi sana  vipodozi kama vile sabuni, mafuta, scrubs, lotion na cream hutengenezwa kwa kutumia mchele kama moja ya kiambato muhimu. 

       👉Siri moja tu ambayo napenda nikumegee ni kuwa kwa kiasi kikubwa urembo wa ngozi ya wajapani, wachina na wakorea inatokana na matumizi ya mchele kwenye masuala ya urembo kwa vizazi vingi. (wao wenzetu wameendelea kuenzi aslili kwa kuendelea kutumia bidhaa zenye viambato vya asili kwenye vipodozi vyao. 

      👉Hii ni tofauti kabisa ba huku kwetu ambapo wakina dada wengi wanajisikia ufahari mkubwa wakitumia vipodozi vyenye kemiekali zenye sumu ambavyo pamoja na kuvinunua kwa gharama kubwa, vipodozi hivyo pia vimethibitishwa kuwa na hatari ya kuleta athari mablimbali za kiafya kama vile saratani na matatizo ya uzazi.

👉👉" kumbuka haya siyo maneno yangu ni tamko lililotolewa na SHIRIKA LA VIWANGO TANZANIA YAANI TBS ambao ndio wanaosimamia ubora wa bidhaa vikiwemo vipodozi kwa hapa nchini. BOFYA HAPA SASA HIVI TAARIFA YA TBS KUHUSU JAMBO HILI

TUENDELEEE NA HISTORIA YETU..

        👉Sababu kubwa ya mchele kuwa na uwezo mkubwa wa kufanya ngozi  yako ing'ae ni kutokana na kuwa na virutubisho vingi ikiwemo Vitamini E ya asili  ambavyo hurutubiusha ngozi hivyo  kuifanya iwe na muonekno mzuri na mrembo wakati wote bila kujalisha umri ulio nao au mazingira unayoishi. 

     👉Kutokana na uwepo wa virutubisho muhimu kwenye mchele, mtu yeyoye ambaye atatumia sabuni iliyotengezwa kwa mchele basi ngozi yake itakuwa na muonekano mzuri na kumfanya aonekane mrembo wakati wote. 

     👉Maana yake ni kwamba tofauti na sababuni za kawaida, ukiogea sabuni iliyotenegzwa kwa mchele pamoja na kuondoa uchafu sabuni hii husaidia kuilinda ngozi yako dhidi ya magonjwa au matatizo mbalimbali. 

 👉 Naomba sasa nikupe sababu kubwa saba (7) zitokanozo na kutumia sabuni ya mchele. 

     Japokuwa kuna faida nyingi sana, leo hii naomba nikumegee FAIDA 7 MUHIMU ZA KUOGEA SABUNI YA MCHELE  kama ifuatavyo. 

  1. Hufanya ngozi yako iwe nyeupe 
  2. Husaidia kuondoa chunusi, makovu na madoa meusi usoni
  3. Huondoa mikunjo na kukufanya uonekane kijanaa
  4. Hufanya uso wako uwe na mwangaza wakati wote hivyo kukufanya uonekane kijana 
  5. Hufanya ngozi yako iwe laini na nyororo wakati wote
  6. Husaidia kuondoa mafuta ya ziada kwenye ngozi yako
  7. Hulinda ngozi yako dhidi ya mionzi ya jua

   Najua inawezekana upo unajiuliza ni namna gani unaweza kupata sabuni ya mchele ambayo ni OG (kumbuka pia mjini hapa kuna wapigaji wengi) wnakwambia kuwa ni sabuni ya mchele kumbe ni uongo mtupu wanakuwa wamechakachua.

Ukitata kupata sabuni ya mchele OG basi hakikisha unatafuta sabuni iliyozalishwa na Kunyumba Natural Produtcs na unaweza kuipata kwa wasambazaji bidhaa zetu KOBOFYA HAPA SASA UPATE NAMBA ZAO


Aidha uaweza kuona bidhaa zetu kwenye duka letu la mndadaoni 



 
AIDHA KAMA UNATAKA KUWA WAKALA WA SABUNI HIZI  KAMPUNI YETU INATOA FURSA HIYO NA TUTAKUPA PUNGUZO KUBWA SANA LA BEI. BOFYA HAPA SASA KUJAZA TAARIFA ZAKO


Maoni

Chapisha Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

ORODHA YA WASAMBAZAJI WETU

FAIDA KUMI ZA KUTUMIA SABUNI NA VIPODOZI VYA ASILI (NATURAL SOAPS AND COSMETICS)