Siri ambayo watu wengi hawaijui
Watu wengi siku hizi hujali afya zao kwa kufanya mazoezi pamoja na kuepuka kula vyakula ambavyo vina kemikali ambazo zinaweza kusababisha madhara ya kiafya kwao. Wengi wetu hutumia umakini mkubwa sana katika vyakula ambavyo tunavila ili kujiridhisha kuwa vyakula hivyo havina kemikali zenye sumu kama zebaki (mercury) ambazo husababisha madhara ya kiafya kama vile ugonjwa wa saratani.
Kitu ambacho naamini watu wengi hawajagundua ni kwamba ngozi zetu ni moja ya njia kubwa sana kuliko njia nyingine yeyote ambayo inaweza kusababisha kemikali zenye sumu pia zinaweza kuingia katika miili yetu.
"Najua unashagaa kusikia hivyo, lakini ukweli ndio huo. Sasa ngoja nikueleze jinsi gani hii inaweza kutokea".
Tafiti zinaonesha kwamba ngozi inachangia zaidi kuingiza sumu mwilini kuliko hata chakula. Hii ni kutokan na na ukweli kwamba ngozi ndio kiungo kinachochukua sehemu kubwa zaidi ya mwili kuliko viungo vingine vyote.
nadhani unakubaliana na mimi kuwa kila siku lazima utumie sabuni au kipodozi katika kuweka miili yetu kuwa katika muonekano mzuri. Tatizo lililopo wengi wetu hutumia sabuni na vipodozi vya kisasa ambavyo kitaalam vinajulikana kama syntetic soaps and cosmetics. Sabuni na vipodozi hivi hutengezwa na kemikali ambazo zinaweza kusababisha madahara ya kiafya. Ndio maana Shirika la Viwango Tanzania (TBS) limepiga marufuku zaidi ya sabuni na vipodozi 100 kutokana na vipodozi hivyo kubainika kuwa na viambato veye sumu kama vile hydroquinone, merqury n.k zilizothibitika kusababisha madhara mbalimbali ya kiafya kama vile saratani, matatizo ya uzazi na kadharika.
Baadhi ya madhara ya kutumia vipodozi vyenye kemikali za sumu
BOFYA HA KUONA ORODHA YA VIPODOZI VILIVYOPIGWA MARUFUKU
Hata kwa vipodozi au sabuni ambazo hazijapigwa marufuku na TBS, bado ili ziruhusiwe kuingia sokoni ni lazima zihakikiwe kuangalia kama hazina kemikali hatari kama vile zinc, mercury, parabens n.k katika kiwango ambacho ni zaidi ya kile ambacho ni salama kwa afya ya binamu.
Kwa mantiki hiyo endapo utakuwa unatumia sabuni au kemikali zenye sumu, maana yake ni kwamba ngozi itakuwa inafyonza kiasi kikubwa cha kemikali na kukiingiza mwilini hivyo kuongeza hatari ya wewe kupata madahara ya kiafya.
Je ufanye nini ili kujiweka mbali na uwezekano wa kupata madhara?
Kwa mmantiki hiyo, ikiwa wewe ni miongoni mwa watu ambao wanajaribu kwa kadri wawezavyo kupunguza uingizaji wa kemikali zenye sumu mwili kwa lengo la kulinda afya yako ni vyema ukafikiria pia kuachana na matumizi ya sabuni na vipodozi vya kawaida (Synthetic Soap and Cosmetics) vilivyopo sokoni kwa muda mrefu na kuanza kutumia sabuni na vipodozi vya asili (Natural Soaps and Cosmetics) kama zile zinazotengezwa na Kunyumba Natural Products. Hii ni kwa sababu sabuni hizi za asili hazina kabisa kemikali hatari kwa kuwa hutengezwa kwa kutumia malihghafi za asili kama vile mimea na wanyama. Ukisoma kwenye lebo ya sabuni hizi utakuta viambato vyake ni majina ya vitu ambavyo unavifahamu kama vile mafuta ya maweze, mafuta ya mise, mchele, ukwaju, kahawa, manjano, mafuta ya nazi, mafuta ya parachichi n.k. vitu ambavyo huwa tuna vila kila siku na hatujawahi kuambiwa kuwa vinaleta madhara kwenye miili yetu. Na hauwezi kukuta kwenye viwango vya TBS eti wameweka ukomo (limits) za vitu hivyo.
Faida za kutumia Sabuni na vipodozi vya asili
Kwa kutumia sabuni na vipodozi vya asili hasa vile vinavyotengezwa na KAMPUNI YA KUNYUMBA NATURAL PRODUCTS utapata faida zifuatazo:-
1. Sabuni za asili kweli ni sabuni
Ukizunguka kwenye maduka mbalimbali au kwenye vibanda mbalimbali utaona kuna utitiri wa vitu vinavyoitwa sabuni za kuogea japo ki halisia siyo sabuni ki ukweli kwa kuwa zinakuwa zimejaa makemikali kibao kama vile rangi za kuvutia, harufu za kuvutia lakini kiukweli siyo sabuni halisi. Na haya siyo mameno yangu ni kwa mujibu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Dawa na Chakula (Food and Drugs Administration - FDA ) wanasema sasa hivi sabuni ni chache sana wengi hutumia vitakasa mwili na siyo sabuni. CHANZO FDA
Hii ni kwa sababu kwenye utenegezaji wa sabuni hizi nyingi zilizopo sokoni. hutumia makapi ya mafuta. Najua unaweza kuwa unashangaa kwa nini nasema hivyyo.
Katika utengezaji wa sabuni viambato vikubwa vinavyoifanya sabuni ni mafuta yeyote ya mmea mfano maweze na kitu kinaitwa caustic soda. Hivi vikichanganywa ndio vinatoa sabuni. Sasa kwa hizi sabuni ambazo zinatumiwa na watu wengi kinachofanyika katika kuzitengeza ni kwanza viwanda vikubwa vinaanza kuchuja mafuta ya kula (refined edible oil) kutoka kwenye mafuta ghafi mfano ya mawese, kishamakapi yanayopatikana yantumika kutengeza margarine halafu baada ya kutengengeza margarine makapi ya mwisho ndio htumika kutengeza sabuni.
Kwa upande wa sabuni za asili. hizi ni sabuni halisi kwa kuwa zinatengezwa kwa kutumia mafuta yenyewe kabisa ya mawese kabla hayachakachuliwa pamoja na kuongeza mimea mingine mfano parachichi, mchele, kahawa n.k. Kwa mantinki hiyo sababu kubwa ya kuzifanya sabuni za asili kuwa ni bora ni kutokana na kutumia maligahfi halisi.
2. Sabuni za asili husaidia kuipa ngozi Afya
Ngozi yetu ni moja ya kiungo kikubwa sana ambacho kina saidia ufyonzaji wa vitamini na madini ambavyo husaida katika kuifanya ngozi kuwa na afya nzuri. Kutokana na sabuni za asili kuwa na vitamini na madini za kutosha (kumbuka kwa kiasi kikubwa zinatengezwa kwa kutumia mimie ambayo kwa asili ina vitamini na madini za kutosha kama vile parachichi, mchele, mlonge, kahawa, ukwaju, manjano n.k) Kwa watu wanaotumia sabuni za asili ngozi yao huwa na afya nzuri sana hii ni kutokana na sabuni za asili kuwa na vitamini vya kutosha.
3. Sabuni za asili huifanya ngozi yako kuonekana changa wakati wote (inazuia ngozi kuoenekana zee)
Katika mchakato wa kutengeneza sabuni za asili kuna kiasi kikubwa sana ya Antioxidant hupatikana kutoka katika malighafi zilizotumika. Antioxidants hizi husaidia ngozi kujitengeneza yenyewe na hivyo kukifanya ionekan changa na safi kila wakati (anti- aging properties).
4. Sabuni za asili zina viuwa vimelea aina ya bakteria (anti- bacterial) vya asili
Sabuni za kawaida tulizozizoea huua vimelea kutokana na kemikali kama vile triclosan, sulfates, parabens n.k , ambazo ndio husaidia kuua vimelea kama bakteria. Pamoja na kuua vimelea kemikali hizi zinaongeza hatari mwili kupata madhara ya kiafya kama vile saratani zingine pamoja na kuathriri mfumo wa uzazi. Kwa upande wa sabuni za asili (natural soaps) zenyewe huua vimelea vya magonjwa kutokana na kemikali za asili ambazo ndizo huua vijidudu au hufukuza vimelea vya magonjwa. Mfano mti wa mkaratusi, mlonge, mwarobaini au mmea aina ya mchaichai kwa asili hutumika kama dawa kwa ajili ya magonjwa mbalimbali. Aidha, itolewayo na mimea kama mchaichai husaidia kufukuza vimelea vya magonjwa kama bakteria katika ngozi yetu.
Hitimisho
Najua fika kuwa wewe unajali sana afya yako na inawezekana ulikuwa unatumia sabuni za kawaida kwa kuwa ulikuwa hauna uelewa wa kwamba unachokitumia sio sabuni na (vitakasa mwili) vinavyoandaliwa kwa kutumia makapi mbaada ya kuonoa virutubishi vyote vya muhimu vinavyohitajika ngozi.
Ni imani yangu kuwa baada ya kutambua kuwa sabuni za kawaida ambazo unazitumia wewe na famili yako zinaweza kuleta athazi za kifaya na kuwa unaweza kuepukana na sabuni athari hizo kwa kutumia sabuni za asili, utafanya mapinduzi makubwa leo na kuanza kutumia sabuni za asili wewe na familia yako. Hata hivyo, nakushauri uwe makini sana na wapi unapata hizo sabuni za asili kwani kuna baadhi ya wafanyabiashara wenye tamaa huwadanganya wateja wao kuwa sabuni zao ni sa asili kumbe sio wa kweli.
Kama unahitaji kupata sabuni za asili za uhakika, tafadhali usisite kuwasiliana nami kwa simu na
BOFYA HAPA SASA KUINGIA KWENYE DUKA LETU LA MTANDAONI. Nakuahidi kukupa sabuni ambazo za asili zenye ubora na zisizo na madhara kwa afya yako. Hata hivyo, kutokana na wingi wa wateja ninaowasikiliza naomba ikitokea unanipigia simu haipokelewi, unitumie ujumbe mfupi kwa njia ya Whatsapp au meseji ya kawaida. Asante Sana.
makubwa kwa kuachana na matumizi ya sabuni za kawaida na kuanza kutumia sabuni za asili hasa hasa zile ambazo zinatengezwa na Kmapuni ya Kunyumba Natural Products.
Maoni
Chapisha Maoni